OUR EVENTS

image

MAHAFALI YA WAANZILISHI Tarehe 03/10/2020 Familia ilifanya mahafali mazito ya kwanza ya Kidato cha Nne waanzilishi 27. Mgeni Rasmi alikuwa Mchg. Dr. Fidon Mwombeki, Katibu Mkuu wa AACC yenye makao yake Nairobi. Alihudhuria Askfofu Mchg. Dr. A. Keshomshahara na Msaidizi wake Dean J. Mushendwa. Katibu Mkuu wa Dayosisi Mchg. E. Kigembe na Mtunza Hazina J. Lwezaura. Wajumbe wa Bodi, Wazazi, majirani, na wakuu wa vituo walifika kwa wingi. Majirani walialikwa watu wasiotambulika mno katika jamii. Tulialika wanafunzi si chini ya wanne kila shule ya msingi jirani. Watu hawa wa kawaida walialikwa kwa sababu familia yetu inalenga kuthamini watoto na watu wa kawaida kwa kuwa wanafunzi wa familia hii pia wanatoka katika familia zisizo maarufu. Tulikula tukanywa na kucheza mbali na hotuba nzuri ya mgeni rasmi iliyosisitiza umuhimu wa elimu kwa watoto. Tunawatakia kila kheri Kidato IV ili wanavyoshinda kitabia, washinde kitaaluma. Mkazo wetu ni Ushindi wa Tabia na kisha ushindi wa Kitaaluma.